Saturday 14 December 2013

STARS WALIVYOTUA DAR KUTOKA CHALLENGE KENYA

Wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars', Himid Mao mbele na Elias Maguri nyuma wakiteremka kwenye ndege ya RwandaAir baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni ya jana wakitokea Nairobi, Kenya walikokuwa wakishiriki Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge ambako walishika nafasi ya nne, huku wenyeji, Kenya 'Harambee Stars' wakitwaa ubingwa.
Wachezaji wakisubiri kukamilisha taratibu za Uhamiaji.
Mrisho Ngassa akifanyiwa taratibu za Uhamiaji.
Kocha Mkuu, Mdenmark Kim Poulsen akiwa JNIA baada ya kuwasili.
PICHA NA BINZUBEIRY.

No comments:

Post a Comment