Monday 9 December 2013

Ulimwengu, Ngassa, hatihati kuivaa Kenya

Stars iliivua Uganda ubingwa wa Chalenji kwa penalti 3-2 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa mjini Mombasa juzi Jumamosi na sasa itaikabili Kenya kesho Jumanne kwenye mchezo wa nusu fainali.
Kocha huyo alisema aliendelea kuwatumia mastraika watatu Mrisho Ngassa,Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa muda mrefu kwa kusudi maalum la kushambulia licha ya Aboubakary Salum kuonyeshwa kadi nyekundu.
Poulsen alisema; “Niliendelea kuwatumia Ngassa, Samatta na Ulimwengu kwa muda ili kutunza mashambulizi ambayo yaliipooza Uganda,ilikuwa ni mechi ngumu na kushambulia ndio kulitusaidia.
“Kuwatoa mabingwa watetezi si kazi rahisi,tumefanya kazi nzuri, timu imecheza vizuri na imefanya Watanzania wanachotaka.
“Tulipoingia lengo ilikuwa ni kufika robo fainali, tumeingia na tukamtoa bingwa mtetezi kila mmoja sasa atakuwa akituangalia sisi, tunaingia kwenye nusu fainali kwa ari ileile,”alisisitiza Poulsen ambaye huenda akamkosa Ngassa na Ulimwengu kwenye mchezo dhidi ya Kenya baada ya kuumia dhidi ya Uganda.
Ngassa na Ulimwengu waliumia katika mchezo na Uganda, Ngassa aliumia kifundo cha mguu na kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Athuman Iddi’Chuji’ wakati Ulimwengu aliumia nyama za paja ingawa aliendelea na mchezo hadi mwisho.
Hatma ya wachezaji hao wawili itajulikana leo Jumatatu timu hiyo itakapofanya mazoezi mepesi mjini Nairobi ikijiandaa kwa safari ya saa mbili na nusu kesho Jumanne kuelekea Machakos itakakopigwa mechi.

No comments:

Post a Comment