Monday 2 December 2013

Berko: Yanga kwangu ni historia



KIPA mpya wa Simba, Yaw Berko kutoka Ghana ametamka kuwa amekuja Tanzania ili kuing’arisha Simba kwenye Ligi Kuu Bara na michuano mingine.
Kipa huyo pia amesisitiza kuwa, Yanga kwake imebaki historia huku akinukuu maandiko ya Biblia: “Dunia kila kitu kitapita, na yeye Yanga alipita na kwa sasa imebaki historia, sasa yeye ni mchezaji wa Simba.’’
Berko, kipa aliyeipa mafanikio Yanga lakini alimalizana nao na kurudi kwao Ghana msimu uliopita kuichezea klabu yake ya zamani ya Liberty Professionals. huyo aliyetua nchini juzi Jumamosi asubuhi ameweka wazi kuwa ataichezea Simba kwa miezi sita tu kulingana na makubaliano yao lakini hadi jana Jumapili mchana alikuwa bado hajasaini.
Berko aliliambia Mwanaspoti kuwa amerejea tena Tanzania kwa lengo moja tu la kuifanya Simba ing’are kwenye mzunguko wa pili na kuipa ubingwa.
“Nimerudi kuifanya Simba ing’are mzunguko wa pili, nina uzoefu na ligi ya Tanzania, nawajua wachezaji na sehemu kubwa ya washambuliaji,’’alisema Berko kipa bora wa Ligi Kuu Bara 2011-2012 alipokuwa Yanga.
Aliongeza: “Naujua ushindani, ninachowaahidi Simba ni kuwa mambo yatakuwa mazuri, tuombeane tuwe wazima kiafya.”
Berko anajiunga Simba ambayo ina makipa wengine, Abel Dhaira, Andrew Ntalla na Abou Hashim.
Kuhusu makipa hao alisema: “Sijui chochote juu ya makipa hao, vyovyote sawa kwani wao wapo kwa ajili ya Simba na mimi nimekuja kwa ajili hiyo hiyo, kikubwa ni ushirikiano.

No comments:

Post a Comment