Monday 2 December 2013

Coastal baba lao Kombe la Uhai


COASTAL Union ya Tanga ndio vinara wapya wa michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu Bara.
Coastal imefanikiwa kulibeba taji hilo lililokuwa likishikwa na Azam baada ya kuibwaga Yanga mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa jana  Jumapili kwenye Uwanja wa Azam, Chamanzi, Dar es Salaam.
Vijana wa Coastal waliandika bao la kwanza katika dakika ya 50 upitia kwa Mohammed Kipanga.
Kipanga alifunga akiunganisha krosi ya Abdallah Waziri. Kipa wa Yanga, Said Ndutu, hakuona ndani, bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake na mashambulizi ya zamu kuliandama kila lango hadi ziliposalia dakika tatu mchezo kumalizika pale, Mahadhi Juma, alipoipatia Coastal bao la pili baada ya kuinasa pasi ya Mohammed Rajabu akiwa ndani ya 18.

No comments:

Post a Comment