Tuesday 3 December 2013

OFISI YA CHADEMA ARUSHA YACHOMWA MOTO

OFISI YA CHADEMA ARUSHA YACHOMWA MOTO

Ofisi ya chadema mkoani Arusha imeponea chupuchupu kuteketea kwa moto baada ya watu wasiofahamika kuichoma moto asubuhi ya leo.

Katibu wa Chadema mkoani Arusha, Bw. Amani Golugwa amesema lengo la mtu huyo inaonekana lilikuwa kuteketeza vifaa na nyaraka zao za kiofisi ila alivyoona muda umeenda ndipo aliamua kuchoma (ceiling board) akiamini kuwa moto huo utasambaa mahali kote lakini wao waliweza kuwahi na kuuzima.

Ceiling board ya chumba kimoja na choo ndio maeneo yaliyoathiriwa ila maeneo yaliyobaki na vifaa vyote ni salama.

No comments:

Post a Comment