Sunday 15 December 2013

HASIRA ZA WANANCHI ZAMKUTA KADA WA CCM MWANZA,ALIWAHI KUWA MWENYEKITI WA CCM MKOANI HUMO

Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndg CLEMENT MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kisesa jijini Mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM ndg Joyce Masunga (maarufu kama Maziwa Fresh) ni kweli kuwa tukio hili limetokea na tunaendelea kufuatilia kupata habari zaidi.

No comments:

Post a Comment