Wednesday 11 December 2013

Sentensi 6 za Samson Mwigamba wa CHADEMA leo Dec 11 2013


k3

Mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.
Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.
Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi inasoma:
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya
1 >> kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.
Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.
Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.

No comments:

Post a Comment