Zitto Kabwe.
MKAKATI WA MABADILIKO 2013
UTANGULIZI: Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi
mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wakuu wa taasisi
wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Wa kwanza aliongoza kwa
miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na kumwachia aliyefuata
ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa 2004 na
kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu
mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi
cha pili.
Tunapenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu
wote waliopita walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa
kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili.
Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye
chombo chetu kikuu cha uwakilishi. Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili
tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kufanya idadi
kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu ambaye ndiye aliyepo hivi
sasa, tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita jumla wakawa 11.
2010 chini ya mkuu huyu huyu wawakilishi wakaongezeka na kuwa 23 na wa
nyongeza 25 na kufanya idadi kuwa 48 kabla ya kupata mwingine mwaka jana
na kufanya sasa wawe 49.
Dk. Kitila Mkumbo.
Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji
pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka
msingi mzuri sana wa kutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia
mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa
madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda
madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate
na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwana
taasisi. Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu
kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea
na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha
ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada
yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa
vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema,
wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili
vilivyoruhusiwa katika mwongozo bali wote wawili walikaa kipindi kimoja
kimoja tu.
Samson Mwigamba.
Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka
huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Tunapenda kuainisha matatizo
hayo kwa uchache kama ifuatavyo:
Wakati tukiufanyia mwongozo
wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi
kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano
mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo,
kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo
yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa
maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki
kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu
wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi
kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari
zisizomithirika kwa taasisi yetu.
Ni dhahiri kwamba uongozi
uliopo umeishiwa mbinu na kuakisi jambo la msingi sana ambalo waasisi
wetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa
uongozi kwenye mwongozo wetu. Kuchoka kwa uongozi wetu kunaonekana
dhahiri katika mipango na mikakati ya taasisi ya miaka kadhaa. Mfano
mwaka 2008 uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa
(maarufu kama Oparesheni Sangara). Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa
kadhaa na hatimaye ikafa kimya kimya. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwa
yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya
zote.
Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia
makao makuu ya mkoa na kwenda kwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo
zinaonyesha kwamba yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na
mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha
nayo yakafa kifo cha mende. Kisha mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya
mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C). Hiyo ilikuwa
inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumla
zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa
njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na
hatimaye kufanya mafunzo kwa viongozi. Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi,
Morogoro na kisha ikaenda kufia Iringa. Mwaka huu viongozi wetu wamekuja
na ugatuaji madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka
kwenye kanda mbalimbali. Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale
viongozi wakuu walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza
matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda
mrefu badala ya kuajiri maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao
kwenye uongozi wa muda. Kitendo hiki kwa peke yake, cha kufeli kwa kila
mkakati unaoletwa na viongozi wetu katika hatua za utekelezaji
unaofanywa na wao wenyewe waleta mkakati, ni kiashiria tosha kwamba
uongozi uliopo umechoka.
Performance yetu kwenye chaguzi ndogo
nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika. Tangu uongozi huu uingie
madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo
kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25. Aidha baada ya
mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenye halmashauri.
Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni
2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni
2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata
viti 7 kati ya 29 (24%). Ni dhahiri mabadiliko yanahitajika kwa kuwa
wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo yale yale.
Tunahitaji mbinu mpya. Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata
katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu
iliyopo mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo
katika kila chaguzi. Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa
mafanikio madogo badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala
tunapojikwaa.
Matumizi ya fedha za taasisi. Hakuna mtu
anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka
watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye
taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada
ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha
ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya
uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna
akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje.
Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni
kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye
mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi
wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu
binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo
hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na
hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka
kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na
Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising,
uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.
Taarifa
za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao
chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na
matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina.
Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya
kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua
wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna
pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa
tumesimama. Kwa kiasi kikubwa mkuu aliyepo anatengeneza mazingira
yaleyale ya mwaka 2005 na 2010 ya kutaka chama kiwe hakina hela ili
ikifika wakati wa uchaguzi kimpigie magoti. Kisha atatoa pesa bila
kumbukumbu zozote na mara baada ya uchaguzi anapeleka lundo la deni na
kudai alipwe hela aliyekikopesha chama wakati wa uchaguzi. Alifanya
hivyo katika chaguzi za 2005 na 2010. Wakati wote wa kampeni za mwaka
2010, kwa mfano, taasisi yetu ilihangaika sana kwa kukosa hata hela ya
kununua maji kwa wajumbe wa ngome. Lakini ajabu ni kwamba baada ya
uchaguzi mkuu wa taasisi na baadhi wa wapambe wake walilete deni kubwa
la takribani shililingi milioni mia tano akiadi kuwa walikikopesha
chama. Taasisi imewalipa pesa zote hizi kwa muda mwaka mmoja. Sasa
anatengeneza mazingira hayohayo kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.
Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama. Wakuu
waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada.
Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na
kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za
kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama lile la
kuanzisha kampuni la uwekezaji la taasisi yetu litakalowekeza kwenye
miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa
miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana.
Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa
hapa jirani juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani
kama wamejifunza chochote.
Njia haramu za kubaki madarakani.
Ili kuhakikisha wakuu wanabaki madarakani, wameanzisha vikundi vikundi
ndani ya taasisi yetu. Siku hizi ni rahisi sana kuambiwa kwenye taasisi
yetu eti huyu ni wa boss na huyu ni wa dogo. Na wale walio wa boss kwa
kuwa boss ndo anashikilia raslimali za taasisi anatumia mfumo haramu
kuwaneemesha watu wake kwa kutumia raslimali za taasisi na kuwakandamiza
wote wanaoonekana wanapishana naye kimtazamo. Jambo hili limewaibua
wachumia tumbo, wapenda madaraka, na vibaraka lukuki wanaokwenda
kujipendekeza kwa wakuu wa taasisi kwa malengo ya kujinufaisha binafsi.
Katika kufanya hivyo vibaraka hao wamekuwa wakiwaendea wakuu wa taasisi
na kuwajaza maneno mabaya dhidi ya viongozi wenzao na kuzidi
kuwafarakanisha viongozi wa juu.
Kuna mchezo umeanzishwa na
wakuu wa taasisi unaitwa ulinzi wa chama uliogawanyika katika makundi
mawili yaani visible na invisible. Visible ni ule unaoonekana ambao uko
chini ya kikosi chetu chekundu ambacho kinajulikana kwa kila mtu lakini
invisible wanajulikana kwa mkuu wa taasisi na mtendaji mkuu peke yake.
Wanafanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa hao wawili na hawajulikani kwa
viongozi wengine wa juu. Ni hawa hawa ambao wanatumika vibaya pale
wanapoleta taarifa za kiintelijensia ambazo zinawahusisha viongozi
wasiopendwa na wakuu na usaliti dhidi ya taasisi. Hakuna kamati maalum
inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua
wanaowataka. Ni katika mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika
vibaya kwa kumshambulia mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia
mitandao ya kijamii na wakuu wanafurahia na kumlipa pesa.
Udhaifu wa utendaji wa mtendaji mkuu. Mtendaji mkuu ni dhaifu mno na ni
mara nyingi sana tumeshuhudia mkuu wa taasisi akifanya mambo ya
kiutendaji kinyume na utaratibu kama vile yeye mwenyewe kuja kwenye
kamati ya makatibu na wakurugenzi na kupangua mipango yao na ku-inject
ya kwake na mtendaji mkuu kuadopt tu kana kwamba yeye hawezi kupanga
mambo ya kiutendaji, hata tunapokuwa kwenye operesheni maalum
tumeshuhudia mkuu wa taasisi ndo akipanga watendaji, posho zao na hata
kusimamia matumizi ya pesa na shughuli mbalimbali za kiutendaji. Udhaifu
wa mtendaji mkuu ni udhaifu wa mkuu wa taasisi kwa kuwa amemteua yeye
mara mbili tena mara ya pili alileta jina moja mbele ya Baraza la juu
kuonyesha kwamba aliridhika na utendaji wake kiasi cha kutotaka
kumpambanisha na mwingine. Lakini baada ya kumpendekeza mara ya pili
ndipo tumeshuhudia yeye kuingilia kati mara nyingi sana mambo ya
kiutendaji kana kwamba anamfichia aibu mtendaji wake. Swali kwa nini
alimteua tena? Jibu lake litakuwa rahisi tu kwamba ni kwa sababu
mtendaji huyu ni passivekwa kila takwa la mkuu wake.
Matumizi
mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi. Taasisi yetu inayo
kamati ya tenda ambayo iko chini ya kamati ya makatibu na wakurugenzi.
Lakini uzoefu unaonyesha kwamba kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya
kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo
wanaojigonga kwa wakuu, wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo
ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, vifaa vya
kueneza taasisi, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa mtendaji
mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yote yanafanywa na wakuu hasa hasa mkuu
wa taasisi bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na
linarahisisha matendo ya kifisadi. Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio
amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua
mwenyewe na ambaye haihojiwi popote. Huu ni mfano wa wazi wa mgongano wa
kimaslahi jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi mkubwa wa taasisi kama
yetu inayojitambulisha katika kupinga vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa
maadili ya uongozi kwa ujumla.
Makubaliano ya kifisadi na mtu
binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi. Hakuna kikao chochote cha
juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa
kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi
inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi
vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu.
Mifumo ya
uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi
wakuu wa taasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka
na mara nyingi bila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua. Mambo
haya yanafanyika mbele ya macho na masikio ya mkuu wa taasisi jambo
ambalo linazidi kuthibitisha kwamba mkuu na mtendaji mkuu wanajuana na
wanafanya kwa kulindana.
NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA MKUU:
Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji
mabadiliko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta
mabadiliko tunayohitaji. Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye
tungemuunga mkono lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko
tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za kiuongozi na zaidi sana awe na
uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko. Tukileta mtu asiyefahamika sana
kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi gani
hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea
kuididimiza taasisi.
Katika kuchunguza ndani ya taasisi
tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi ana sifa zote tulizozitaja
hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni dhahiri pia kwamba
udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu aliyepo.
Kwa ujumla mtendaji mkuu:
Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi.
Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa
tumeshuhudia akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia
ya posho ama vinginevyo.
Anaheshimika na viongozi wa ndani na
nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ustawi wa taasisi na
kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa wengi sana kutoka nje
ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika kuhakikisha
tunafanikisha lengo la taasisi.
Ni msomi wa kiwango cha juu na
mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa,
kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatari
kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo.
Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama.
Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu
ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa
hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano
ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani,
kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa
taasisi haraka iwezekanavyo.
Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi
ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa. Tunahitaji kuja na vyanzo vipya
vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu aliyepo si kwamba ameishiwa
bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi kimapato kwa ajili ya
malengo yake ya mbele.
Exposure kubwa na kukubalika katika
siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi ambaye anazifahamu siasa za
kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa. Ni
hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya taasisi yetu bila
mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa. Mpaka hivi sasa
hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na
jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo ‘too local’ na hana
mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na
kimataifa. Ndio maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa
hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa. Hata katika kutoa maoni
katika mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa
kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi tulio nao, nafasi ya taasisi yetu
katika nyanja za kimataifa haipo!
Aina na staili ya uongozi wa
sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo hadi taasisi yetu
itakapochukua dola. Yaani tunafanya mambo kama kwamba tutaanza upya
kabisa tukichukua dola. Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu katika
utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba
tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni
ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu. Ni
kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani
kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi,
n.k.
Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali,
wafanyabiashara wakubwa, watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika
kupata muunganiko wa mawazo na kutoka na sera murua zinazogusa kila
sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda sambamba na kutoa elimu kwa wote
waelewe na watuunge mkono. Tunasema hivi kwa kuwa watu wa kada
mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano
wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk
na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa
uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya
kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank
kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili
wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na
wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.
Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo
yanayohitaji mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza
kuleta mabadiliko tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa
kuutafuta ukuu wa taasisi yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo.
SWOT ANALYSIS:
Kwa kutumia uchambuzi huu hapa chini wa uimara, udhaifu, fursa na
vitisho ama vikwazo dhidi ya mtu tunayempendekeza, utaweza kutuonyesha
kama tunayempendekeza ataweza kushinda vita iliyo mbele yetu. Kama SWOT
inavyotaka, tutaangalia sifa njema alizonazo tunayemtaka ambao ndio
uimara wake, tutaangalia pia udhaifu wake, tutaangalia fursa alizonazo
na mwisho tutazingatia vitisho ama vikwazo vilivyopo. Ni muhimu
tukaeleza kwamba katika SWOT analysis tunajikita kwa mambo yanayohusika
moja kwa moja na uwezekano wa tunayemtaka, kuchaguliwa. Kwa hiyo kwa
mfano utakuta kwamba katika sehemu hii hatutazungumzia sifa njema
alizonazo tunayemtaka kama kiongozi lakini sifa hizo zikawa hazina
ushawishi wa kuwafanya wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua.
Uimara wa tunayemtaka:
Ingawa si mmoja wa waasisi wa taasisi yetu, lakini ni mwana taasisi
mkongwe akiwa amejiunga na taasisi yetu miaka miwili tu tangu ianzishwe
na mwaka mmoja tangu isajiliwe rasmi na serikali.
Zaidi ya kuwa
mwanataasisi mkongwe, hajawahi kujiunga na taasisi nyingine hapo kabla.
Alijiunga na taasisi hii kabla hata haijajulikana kwa watu na alibaki
kuwa mwana taasisi mwaminifu hata pale taasisi zingine zilipoonekana
kuwa imara na maarufu zaidi ya hii.
Kutokana na vipengele ‘a’
na ‘b’ hapo juu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kusema mtu huyu alikuja
kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kutafuta maslahi kama vile uwakilishi
kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi hapa nchini.
Ni
mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea
kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia.
Mahali ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki
kuvumilia mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa
wanadanganywa kwamba mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka.
Ana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi.
Ana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii,
utamaduni, michezo, nk. Uwezo wake unachagizwa si tu na elimu yake ya
darasani bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa.
Ni mzalendo wa
hali ya juu anayeipenda nchi yake kwa moyo wa dhati. Amethibitisha hilo
kwa namna anavyolitetea taifa letu katika medani za kimataifa na jinsi
anavyolipigania ndani dhidi ya mafisadi na wasiolitakia mema taifa letu.
Ni mwakilishi pekee aliyekuwa tayari kukosa mishahara ya miezi kadhaa
kwa kuamua kusimamia ukweli kwamba kuna ufisadi ulifanyika mpaka
akasimamishwa uwakilishi wake kwa mikutano kadhaa ya chombo chetu cha
uwakilishi.
Katika kuzidi kuonyesha alivyo mzalendo tunaweza
kusema hapa kwamba ni kiongozi pekee kutoka upande huu ambaye ameonekana
sana kwenye mambo ya kitaifa kwa mfano kulipigania taifa letu katika
mambo ya kimchezo, kutumia gharama zake kwenda nje ya nchi na kujifunza
mambo mbalimbali yanayoweza kulisaidia taifa katika sekta nyeti kama
mafuta, gesi na madini, nk bila kusahau kwamba amekuwa ndiye mwakilishi
pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifu
ndani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi.
Mambo hayo tuliyoyataja kwenye vipengele ‘e’, ‘f’, ‘g’ na ‘h’ yamemfanya
kuwa kiongozi wa kwanza kuwa maarufu sana katika taasisi yetu
aliyewapiku hata viongozi wa serikali kwa umaarufu. Hii ya umaarufu ni
sifa muhimu sana linapokuja suala la uchaguzi.
Uwezo wake wa
kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi. Hata pale anapokuwa
amepakwa sana matope na wenzake, anapopewa nafasi ya kujieleza huweza
kuwashawishi watu wengi wanaomsikiliza. Hii itamsaidia sana siku ya
kujieleza mbele ya kikao cha uchaguzi ambapo ataweza kupangua hoja zote
dhaifu za kumpaka matope.
Ana uwezo wa kuchangamana na makundi
yote ambapo vijana humwona kama mwenzao, wanawake humwona kama mtetezi
wao wakati wazee humwona kama kijana mwenye busara anayeweza kuelekeza
kama kiongozi.
Ana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa
ngazi za chini kutokana na ziara nyingi alizozifanya na kukutana na
viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Mahusiano
haya mazuri yanachagizwa na jinsi anavyotumia muda wa kuongea na
viongozi wa ngazi za chini kuzungumza kwa lugha ya upole na kuelekeza
viongozi wenzake bila kuwaonyesha dharau.
Si mtu wa kujipenda
nafsi na katika kupambana umaskini wa watu badala ya umaskini wake,
alifikia kuzikataa posho wanazolipwa wawakilishi wakati wakitekeleza
majukumu ambayo kwayo wanalipwa na kuiomba ofisi ya chombo hicho
kuzipeleka posho hizo kwa watu maskini.
Ana limu nzuri sana aliyoipata katika vyuo vinavyoeleweka kitaifa na kimataifa
Ni kijana na hii ni taswira njema kwa sababu taasisi yetu inaungwa mkono sana na vijana
Udhaifu wa tunayemtaka:
Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira
gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia
kukubalika kwake taratibu.
Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo
pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na
wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake.
Hali ya ndoa ya tunayemtaka kutoeleweka msimamo wake
Kuna wakati tunayemtaka hu-respondkwa taharuki kubwa dhidi ya
mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi
yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka
huonekana kufanya maamuzi kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na
kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake
kabla ya kurespond.
Jambo lililoelezwa katika ‘d’ hapo juu
humfanya tunayemtaka wakati mwingine kuonekana ana jazba sana kwa sababu
akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali kwenye taharuki huwa ni
rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana.
Ustahimilivu: yaliyotajwa katika ‘d’ na ‘e’ hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi.
Uwazi:
Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi
wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika
jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi
ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa
utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango
fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.
Fursa alizonazo tunayemtaka:
Utamaduni wa taasisi yetu wa kubadilisha wakuu wa taasisi kila baada ya
vipindi vifupi ili kuleta maono mapya kwenye taasisi unampendelea
tunayemtaka.
Udhaifu ulioonyeshwa na uongozi uliopo chini ya
mpinzani wetu katika kutekeleza program mbalimbali za taasisi nyingi
zikiwa zimebuniwa na wao wenyewe, pia ni fursa kwa tunayemtaka.
Udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na uongozi uliopo kwenye ugawanyaji wa
raslimali za taasisi kama vile fedha za ruzuku, michango mbalimbali ya
wahisani na hata vifaa vya uenezi.
Kujitokeza kwa tunayemtaka
kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya mabadiliko makubwa na
kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya kabila fulani
ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi.
Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea
2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya
uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka.
Imani ambayo
wana taasisi wengi wanayo kwake. Utafiti mdogo unaonyesha kwamba bado
jina la tunayemtaka linatamkika sana midomoni mwa wanataasisi pale
wanapotajwa viongozi wa juu wa taasisi yetu. Hii inaonyesha bado wana
taasisi wanayo imani kubwa kwake na kwa hiyo atakapopata fursa ya
kupangua matope aliyopakwa atakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa.
Mpinzani wetu hana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje
ya chombo cha uwakilishi. Hakuonyesha utendaji wowote wa pekee
alipokuwepo kwenye chombo mwaka 2000 -2005 na hata alipopewa uongozi wa
upande wetu ndani ya chombo tokea 2010 hadi leo 2013 hajafanya lolote la
kutukuka ndani ya chombo hicho.
Mpinzani wetu hana uwezo
mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni,
michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia vipaji
na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake.
Uzalendowampinzani wetu unatia shaka akiwa hajaonyesha lolote la maana
katika kulitetea taifa letu kimataifa. Ingawa ameshapata nafasi lukuki
ya kwenda nje ya nchi lakini mara zote akifika huko ni kuiponda tu nchi
yake. Ingawa anayo majukwaa ya kufanya hivyo akiwa ameshakuwa mwakilishi
mara mbili kwenye chombo chetu lakini hatujawahi kumsikia akiibua
kashfa mahsusi ya ufisadi na kuisimamia zaidi ya yeye mwenyewe wakati
fulani fulani kutuhumiwa kwa ufisadi mfano pale alipokopa kwenye shirika
la umma na kugoma kulipa mkopo.
Katika kuzidi kuonyesha
uzalendo hafifu wa mpinzani wetu tunaweza kuangalia jinsi ambavyo
mpinzani haonekani kwenye mambo ya kitaifa. Hii ni fursa kwa
tunayemtaka.
Mpinzani wetu si maarufu akilinganishwa na
tunayemtaka na hivyo kumpa fursa zaidi tunayemtaka kumshindani mpinzani
wetu kwenye uchaguzi.
Uwezo wa mpinzani wetu wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi ni mdogo sana.
Mpinzani wetu hajazoea ushindani na changamoto. Ni mtu aliyezaliwa
kwenye utajiri na anadhani pesa ni kila kitu. Ukimnyang’anya pesa
ukamwambia ashindane kwa hoja hawezi na ndo maana anajaribu sana
kuhakikisha anaingia mwenyewe ulingoni bila kupingwa.
Kutokana
na tuliyoyasema hapo juu kwenye ‘m’ ni dhahiri kwambapale mpinzani wetu
anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama
anapewa nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka.
Mpinzani wetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo
vijana humwona kama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama
malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona
kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni
waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine.
Mpinzani wetu hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za
chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokukutana na
viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Hutumia
muda mwingi kuwaponda viongozi wenzake hata kufikia kutamka mara nyingi
kwamba kama kiongozi hawezi kujigharamia nauli na malazi ya kutoka
mahali fulani kwenda mahali fulani kwa siku kadhaa hafai kuwa kiongozi
bila kujali kwamba kuna viongozi wetu wana moyo na taasisi hii na ndo
wameifikisha hapa ilipo lakini hawana uwezo wa kifedha na hivyo kauli
kama hizo za mkuu huyu huona kama anawadharau kwa kuwa yeye ni tajiri.
Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi ya chini hivi sasa
na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo amekuwa na
mkakati unaoitwa kuondoa watu wa zamani. Jambo hili linawaudhi sana
viongozi wa ngazi za chini ambao wanaona kama baada ya kuifikisha
taasisi mahali ilipo kwa sasa wanaonekana hawana maana tena. Wengi
wamefikia kuapa kwamba kama mwendo ni wa kuwaondoa watu wa zamani basi
na yeye ni wa zamani lazima aondoke.
Mpinzani wetu amejionyesha
dhahiri kujipenda na kujijali nafsi bila kujali watu wa hali ya chini.
Matukio mawili yanamwacha uchi katika hili pale alipolitangazia taifa
kwamba wawakilishi wetu wote hawatachukua posho za vikao halafu yeye na
wengine wote wanazichukua hadi leo na kumwacha mtendaji msaidizi peke
yake. Na la pili linalofanana na hilo ni pale alipotangaza kutotumia
gari la serikali ambalo ni la kifahari kisha akalirudia kimya kimya.
Kuwepo muhtasari wa kikao cha wazee ambacho mwaka 2009 kilimshauri
tunayemtaka ajitoe na kumwachia mkuu aliyepo na kumtaka mkuu aliyepo
kumwachia tunayemtaka katika uchaguzi ujao na wote wakasaini makubaliano
hayo, nayo ni fursa muhimu sana kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo
anaamini kwamba ameshamsambaratisha tunayemtaka na hivyo kwa sasa
amebweteka na hiyo inatupatia sisi fursa kuendelea kuimarisha mtandao
wetu.
Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa
mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani
waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.
Elimu ndogo
na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa
sasa. Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi
kubwa asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa
kuwa na wasomi waliobobea katika kila nyanja. Hii ni kejeli hasa kwetu
sisi ambao tumekuwa tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo’ inaongoza
akili kubwa. Kimsingi tumekuwa tukijisema kwa kukubali kuongozwa na mtu
mwenye akili ndogo.
Mkuu wa sasa kutokuwa na msimamo thabiti
katika mambo ya msingi. Rejea swala la maandamano ya kumshinikiza
Kawambwa ajiuzulu na kujitoa katika mchakato wa katiba.
Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka
yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda
tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana
na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.
Utayari wa
mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya
kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more
genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya
vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa
tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila
maelezo yoyote
Kitendo cha mkuu aliyepo kung’ang’ania kuendelea nayo
ni kikwazo kwa kuwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima
amejipatia watu wanaomhusudu ama kumpenda ama kumkubali na kuwepo
wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo akitoka taasisi itakufa hata
kama hawana sababu yoyote.
Tunatazamia mkuu aliyepo atafanya
vitendo vingi zaidi vya haramu katika kumdhibiti tunayemtaka pale
tunapoelekea kwenye uchaguzi wenyewe.
Raslimali za taasisi
kutumiwa na viongozi waliopo katika kumsaidia mkuu aliyepo wakati wa
kwetu anatumia raslimali zake za mfukoni.
Propaganda chafu zilizokwishapigwa dhidi ya tunayemtaka zimepunguza imani ya wanataasisi kwa tunayemtaka kwa kiasi fulani
Baadhi ya mambo ambayo amekwishayasema ama kuyatenda nayo yameshawapunguzia imani kiasi fulani wanataasisi mbalimbali.
Kutoonekana sana kwenye operations za taasisi yetu pia kumewapa wasiwasi baadhi ya wanataasisi.
Muhtasari wa SWOT analysis unaonyesha kwamba strength na opportunities
za tunayemtaka ni nyingi sana zikilinganishwa na weaknesses zake na
threats dhidi yake. Aidha ukichambua zaidi utaona kwamba weaknesses za
tunayemtaka nirepairable na vikwazo dhidi yake pia ni rahisi kuvikabili
na kuvisambaratisha. Tukishamaliza maandalizi ya mkakati huu tukaonana
na mhusika mkuu na kumpa ushauri akatulia na kufanya kazi, mkuu aliyepo
hatafua dafu. Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu
aliyepo aendelee kubweteka na ndiyo maana hata lugha iliyotumika ni
ndani hapa ni ya pekee. Tunahitaji tunayemtaka asionekane kama kuna kitu
anafanya na tunafurahi kwamba kuna wakati alitangaza kwamba hana nia ya
kugombea tena waliopo wanatosha. Ikitokea vyombo vya habari vikamuuliza
tena hiyo ndiyo iwe kauli yake ili kuendelea kumfanya mkuu aliyepo
asihangaike na hivyo kuja kummaliza kirahisi. Aidha katika utekelezaji
wa mkakati kama tutakavyoeleza hapo baadaye, tunayemtaka atajitenga
mbali asionekane hata kuwa karibu na sisi. Vikao vyetu na yeye
vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi
ikiwezekana hata nchi jirani.
Mkakati huu hautatakiwa
kupatikana kwenye komputa zaidi ya tatu yaani ya mchapaji ambaye ni M3,
ya M3 na ya MK mwenyewe. Hata hivyo email zitakazotumika kusafirisha
mkakati huu kutoka kwa M3 kwenda kwa M1 hadi kwa MK hazitakuwa zile za
kawaida za hao watu bali mpya kabisa zilizofunguliwa kwa makusudi haya
tu na kwa majina fictitious. Aidha kila atakayekuwa na mkakati huu
kwenye computer yake anatakiwa kuliwekea file hilo password ili hata mtu
wa karibu naye anayeweza kufungua computer yake asiweze kulifungua file
hilo. Pia email address hazitatolewa kwa sms bali kwa kupiga na
kuambiana spelling za address.
MTANDAO WA USHINDI:
Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa
tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa
anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga
kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu
kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo
mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata
wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la
mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa
simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye
kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya
kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa. M2 ni
mtu ambaye yuko kwenye ofisi kuu za taasisi yetu wakati M3 ndiye
mchapaji wa mkakati huu.
Kamati hii imefanywa kuwa na members
wachache sana wenye uelewa mpana wa mambo na wenye elimu nzuri ili
kuhakikisha kazi inafanyika kitaalam na kwa uhakika sana. Kamati ya
kitaifa itapeleka mapendekezo yake kwaMM na yeye pia ataleta ushauri
wake kwa kamati kama mishale inavyoonyesha. Chini ya kamati ya kitaifa
kutakuwepo waratibu wa kanda zote kumi watakaojulikana kama MK1 – MK10.
Hawa watatafutwa na kusimikwa na kamati ya kitaifa kwa kushauriana na MM
kwa utaratibu utakaokubalika na pande zote yaani MM na kamati ya
kitaifa. Chini ya waratibu wa kanda kutakuwapo waratibu wa mikoa yote 30
(MMK1 – MMK30) ambao watapatikana kwa utaratibu ule ule wa kuwapata
waratibu wa kanda. Isipokuwa pale ambapo inakuwa ngumu, itabidi kamati
ya taifa isaidiane na waratibu wa kanda kuwapata waratibu wa mikoa
lakini kamati itashauriana na MM kabla ya kuwasimika rasmi hao waratibu
wa mikoa.Mtandao utakuwa kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro ufuatao:
NAMNA YA KUFANIKISHA MKAKATI:
Kazi itagawanywa katika awamu tatu: Awamu ya kwanza ni
kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza. Katika awamu
hii kazi ni kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye
ngazi ya mkoa. Kazi nyingine itakayofanyika ni kwa waratibu wa mikoa
kuendelea kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo
tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya
mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi
kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye
uwezo wa kutunza siri. Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa
kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa
kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya
kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema
kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero.
Awamu ya
pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa
unapokamilika. Katika awamu hii tutasaidiana na waratibu wa kanda na
mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao
kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili
waje wawachague kwenye wilaya.Vivyo hivyo kwa makada tuliowaspot kwenye
mikoa wahakikishe wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili
nao waje wawachague kwenye mikoa yao. Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya
mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa
ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80.
Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi
uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa. Katika kipindi hiki kwa ustadi
mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja
kufanya mabadiliko makubwa kitaifa. Ni wakati huu ambapo tutawaingizia
mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye
kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko. Ni katika kipindi hiki ambapo
kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao
hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na
kuwarecruit kwenye mkakati.
Aidha katika awamu zote tatu kazi
ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba
mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao
watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha
tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia
nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi.
MAHITAJI YA KUFANIKISHA MKAKATI: Raslimali watu.
Tunahitaji watu waaminifu watatu kwenye ngazi ya kitaifa ambao tayari
wapo. Tunahitaji watu waaminifu kumi kwenye kanda ambao tutawatafuta na
pia waaminifu wengine 30 kwenye mikoa yote thelathini.
Fedha.
Tunahitaji fedha kwa ajili ya mawasiliano kati ya wanakamati na wale wa
ngazi ya chini. Aidha tunahitaji fedha kwa ajili ya gharama za usafiri
pale tutakapohitaji kwenda kwenye kanda na mikoa husika kwa ajili ya
kusimika watu hao tunaowahitaji.
MAPENDEKEZO MAHSUSI NA HITIMISHO: Katika kuhitimisha tunapendekeza mambo mahsusi yafuatayo:
Kuhusu Bajeti:
Tunapendekeza kwamba bajeti ya mkakati huu isipangwe hivi sasa. Ni
muhimu tu sote kuelewa kwamba wakati wenzetu wanatumia raslimali za
taasisi kujijenga na kutekeleza mkakati wao wa ushindi, sisi tunapaswa
kuingia mifukoni. Kwa kila kila mmoja wetu atakuwa budget conscious ili
kuepuka matumizi makubwa ya pesa. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba
lazima pesa inahitajika ni muhimu M1 na MM kujaribu kuangalia namna ya
kuraise pesa na kushauri. Otherwise, tutakapokuwa tunahitaji kufanya
hatua yoyote ama jambo lolote tutakuwa ndo tunapiga hesabu za funds
tunazohitaji kwa jambo husika na kuingia katika utekelezaji.
Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao
utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:
Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao
vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Aendelee kushusha ‘nondo’ ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na
kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye
maslahi ya kitaifa.
Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale
anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na
wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke
kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito.
Sambamba na ‘iv’ hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila
kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na
vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile
tulichokizungumza kwenye kipengele cha ‘iv’ hapo juu.
Kuhusu mapambano ya kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii: Katika hili sisi hatukuona haja ya kufanya hivyo kwa sababu mbili:
Imani yetu kwamba taasisi yetu ni kubwa kuliko watu kwa hiyo ni muhimu
kuzingatia kwamba hatuiui taasisi katika mapambano haya. Tukiendekeza
mashambulizi kwa njia ya mitandao ya kijamii hatutakuwa na ngao ya
kuwakinga watu wa kawaida (wanataasisi na wasio wanataasisi) dhidi ya
kujikuta wakiamini kwamba taasisi hii nayo haina jipya ni sawa tu na ile
tunayotaka kuitoa.
Tutakuwa tumeiua taasisi na mkakati huu
hautakuwa na maana sana kama lengo ni kufanya mabadiliko ya uongozi wa
taasisi tu lakini malengo ya taasisi ya mwaka 2015 yasitimie!
Kujikita kwenye mashambulizi kupitia mitandao ni kuzidi kuwashtua wakuu
waliopo kwamba bado tuko serious na mkakati wa kuwatoa na kuwafanya
wafanye kazi zaidi huku wakiendelea kumpaka matope MM kwamba ndiye
anayerusha makombora hayo kwenye mitandao kwa kusudi la kuhujumu taasisi
maana hiyo ndo lugha yao. Hatukatai kwamba wakuu wanajua kabisa kwamba
bado MM ana nia ya kumvaa mkuu aliyepo lakini tunajua kwamba kwa sasa
wanaamini wamemdhoofisha na hana madhara tena. Ndiyo maana tunataka
kutekeleza mkakati wetu kwa siri sana ili wafikiri MM amekata tamaa
kumbe ndo anakuja na mkakati mzito zaidi.
Hata hivyo, ni muhimu
kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha
kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea!
Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars’
na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy
kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na
kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi. Atakayefanya
kazi hiyo ni sisi wengine wala si yeye! Pia tutahakikisha kila post ya
kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema
aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa
ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia
kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani
kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa
karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu.
Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3):
Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu
tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa
mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu
wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba
M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo. Ni
katika mwendelezo huo huo tunamwona M2 naye akiwa ukingoni kupigwa nje
na kuachwa mtupu na wakuu waliopo katika kile wanachokiita wao reshuffle
ya ofisi kuu. Kwa sababu hiyo tukapendekeza kwamba MM kwa kushirikiana
na M1 kwa hatua ya kwanza wanaweza kutafuta kiasi cha sh. 2m kila mmoja
tukijua kwamba kama members hawa wawili wakisaidiwa milioni mbili mbili
wanaweza kuanzisha projects ambazo zitawasustain hata kama hawana ajira.
Kwa hatua ya baadaye tutasaidiana kuona kama hawa members wanaweza
kusecure good employments mahali, provided hazitawazuia kufanya siasa.