Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed
amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye mamlakani amewahi kufikishwa
mbele ya mahakama ya ICC. Taarifa hii bila shaka imetafsiriwa na wengi
kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru Kenyatta kuwasilishwa mbele
ya mahakama ya ICC mwezi ujao.
Duru zinseama kuwa kuwa hofu kuwa huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama. Waziri Amina amesema kuwa Rais Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa yeye ni rais hali imebadilika. Kenyatta anatakikana na mahakama ya ICC kuhusiana na uhalifu dhidi ya bindamu katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008
Bi Abdalla aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.
Wakati huohuo, Kenya imekanusha madai kuwa inashinikiza mataifa mbalimbali ya Afrika kujiondoa katika mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC.
Waziri wa mashauri ya kigeni nchini humo balozi Amina Mohamed kuwa Kenya imekuwa ikishirikiana na mahakama hiyo na hata Naibu wa Rais William Ruto kwa sasa yuko mjini the Hague kuhudhuria vikao vya hakama hiyo.
Matamshi ya Bi Amina yanatukia siku chache tu kabla ya mkutano wa Marais wa Afrika utakaofanyika Ethiopia jumamosi hii. Bi Amina alisema kuwa Kenya haijashinikiza nchi yoyote kuondoka kwenye mkataba wa Roma na kuwa mkutano wa AU umeitishwa na nchi mbili tofauti wala sio Kenya.
Kadhalika Amina amesema kuwa Kenya haina nia yoyote ya kutoendelea kushirikiana na mahakama ya ICC.
Wakati huohuo mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai amepewa fursa ya kuielezea mahakama ya ICC kwa nini bunge la Kenya lilipitisha hoja ya kuitaka Kenya kujiodnoa kutoka katika mkataba wa Roma.
Majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto, walisema kuwa maelezo ya Muigai yatasaidia mahakama kuchukua hatua zaidi za kuwalinda mashahidi ambao tayari wametoa ushahidi wao.
Jaji mkuu anayeongoza jopo la majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya Ruto, Chile Eboe-Osuji,ambaye alielezea kuwa wanajadili swala hilo na kuwa maelezo ya Muigai kuhusu mkakati wa serikali kutaka kuiondoa Kenya kutoka katika mahakama ya ICC utawasaidia kufanya uamuzi.
No comments:
Post a Comment