Monday, 7 October 2013

MAHARUSI WATIWA MBARONI DAKIKA 3 BAADA YA KUFUNGA NDOA

 
Ndoa hiyo iliyotawaliwa na usiri mkubwa, ilifungwa nyumbani kwa bibi wa mwanafunzi huyo aitwaye Asha Abdallah maeneo ya Tandale Kwamtogole, Dar.
Kuvuja kwa siri ya ndoa hiyo kulifanikishwa na mmoja wa ndugu wa familia ya mwanafunzi huyo ambaye alidai kitendo hicho kilimkera hivyo kuwaomba mapaparazi wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) iliyo chini ya Global Publishers kumnusuru binti huyo mdogo aliyedaiwa kulazimishwa kuolewa.
Baada ya kumsikiliza kwa umakini ndugu huyo mwenye mvi za hekima, mapaparazi wetu walilishirikisha jeshi la polisi na kuanza kuwafanyia mtego wa kuwanasa waliokuwa wakifanikisha tukio hilo.Mishale ya saa 4:00 asubuhi kama ilivyoripotiwa na mtoa habari wetu, tayari bwana harusi ambaye ni fundi seremala alikuwa akiwasili ukweni na kupokelewa na nderemo za chinichini huku mapaparazi wetu wakiwa wamezingira eneo hilo.
Mapaparazi wetu walifanya upekepeke na kuingia hadi chumba cha bi harusi mtarajiwa na kumkuta shangazi yake akimpamba fastafasta kwa kile ilichoonekana kama walichelewa kumaliza kazi hiyo hadi ndoa inaanza Mishale ya saa 4:00 asubuhi kama ilivyoripotiwa na mtoa habari wetu, tayari bwana harusi ambaye ni fundi seremala alikuwa akiwasili ukweni na kupokelewa na nderemo za chinichini huku mapaparazi wetu wakiwa wamezingira eneo hilo.
Mapaparazi wetu walifanya upekepeke na kuingia hadi chumba cha bi harusi mtarajiwa na kumkuta shangazi yake akimpamba fastafasta kwa kile ilichoonekana kama walichelewa kumaliza kazi hiyo hadi ndoa inaanza kufungwa.kufungwa.


 Mambo yakiwa yamenoga huku polisi wakisubiri wahusika wamalize mambo yao, inspekta wa jeshi la polisi aliyevalia kiraia akiwa na ‘mkwaju kiunoni’ alisimama na kujitambulisha kwa jina la Inspekta Rodger na kuwaweka chini ya ulinzi bwana harusi, ustaadhi, bi harusi, bibi yake na ndugu wengine waliokuwa eneo hilo.
Wote wakiwa chini ya ulinzi, Inspekta Rodger aliwatajia tuhuma zao na kuwaita vijana wake waliotanda eneo hilo na kuwaamuru kuwakamata watuhumiwa wote na kuwatia kwenye ‘difenda’ msobemsobe kwa ajili ya safari ya kuelekea Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar kutoa maelezo.




No comments:

Post a Comment