Friday, 4 October 2013

Mambo Shuari Rwanda na TZ, asema Kikwete


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kuwa mgogoro baina ya Tanzania na Rwanda umemalizika.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa raia wa nchi hiyo Rais Kikwete amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina ya viongozi hao wawili yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda .apo hajataja ni kwa namna gani mgogoro huo uliokuwa umefukuta baina ya Tanzania na Rwanda utakuwa umepatiwa ufumbuzi, Rais Kikwete amesema hatua ya mazungumzo baina yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame ndio chanzo cha mafanikio hayo yote.
Tanzania na Rwanda zilingia katika mgogoro wa kidiplomasia hadi kufikia hatua ya kutunishiana misuli kisiri baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzishari nchi za Rwanda na Uganda kuzungumza na waasi wa nchi zao waliopo nchini Jamuhuiri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Jambo hilo lililopingwa vikali na Rwanda kwa madai kwamba Rais Kikwete aliingilia mambo ya ndani ya Rwanda kwa kuwashauri kufanya mazungumzo na watu walioua raia wa nchi hiyo.
Mgogoro huu ulipamba moto na hata kukolezwa zaidi na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Rais Kikwete ametoa wito kwa vyombo vya habari, wanasiasa pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kwa upande mwingine kuziba ufa wa uhusiano uliojitokeza kati ya nchi hizo mbili.
Aidha katika hotuba rais Kikwete alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa opereshi ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini humo iliyofanyika hivi karibuni ambapo amesema kuwa operesheni hiyo iliendeshwa bila kukiuka haki za binadamu.
Kuhusu wahamiaji waliokaa nchini Tanzania muda mrefu Rais Kikwete amesema watu hao sasa watepewa uraia rasmi wa Tanzania ili wafuate uratibu.

No comments:

Post a Comment