Monday, 7 October 2013

Tottenham yaadhibiwa nyumbani

Wachezaji wa West Ham
Ravel Morrison ndiye aliyefunga bao la tatu na la ushindi kwa timu ya West Ham ilipoiadhibu Tottenham 3-0.
Hakuna mtu aliyetarajia kwamba Tottenham wangechapwa namna hivyo hasa kwa kuzingatia kuwa ndiyo iliyovunja rekodi ya pesa nyingi za kuwanunua wachezaji wapya.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kimemalizika kwa timu mbili kutoshana nguvu kabla ya kijana Winston Reid kuingiza bao la kwanza kunako dakika ya 66 na Ricardo Vaz Te akafunga bao la pili dakia sita baadae.
Huo ni ushindi wa kwanza wa West Ham kwenye uwanja wa White Hart Lane tangu mwaka 1999 na ni ushindi wa kwanza wa ugenini tangu msimu huu kuanza.
Katika matokeo mengine Chelsea nao walipata ushindi ugenini kwa kuichapa Norwich mabao 3-1.Southampto waibugiza Swansea 2-0 na West Brom ilitoka sare na Arsenal ya bao 1-1.
Mechi ya mwisho jumamosi usiku ilishuhudia ushindi wa Manchester United wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Sunderland.

No comments:

Post a Comment