Kenya imetoa majina ya wanaume wane ambao inasema
walifanya shambulio dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi
majuma mawili yaliyopita ambapo watu zaidi ya 60 waliuwawa.
Wanaume hao walionekana kwenye picha za kamera za usalama zilizopatikana Westgate baada ya jumba hilo kuvamiwa kwa siku nne.Msemaji wa jeshi aliwataja wanaume hao kuwa Abu Baara al-Sudani, Omar Nabhan, Khattab al-Kene na Umayr.
Alieleza kuwa wote waliuwawa.
Mmoja alikuwa raia wa Kenya.
Kundi la al-Shabaab la Somalia limesema ndilo lilofanya shambulio la Westgate.
Hapo awali wakuu wa Kenya walisema kuwa wapiganaji 10 hadi 15 walivamia jengo hilo.
No comments:
Post a Comment