Kundi la wanawake walivamia nyumba ya mwanaume mmoja wa makamamo ambaye inaaminika kuwa amempa mimba mtoto wake wa darasa la sita. Wanawake hao walienda nyumbani kwa Samson Momposh ambako mtoto wake analea mtoto wa mwezi mmoja.
Momposh anakabiliwa na tuhuma ya kulala na mtoto wake wa darasa la sita na kumpa mimba madai aliyoyakataa.
Mtoto wake na mke wake walipata mimba wakati mmoja na kwasasa wote wana watoto wenye umri unaokaribiana sana ambao inadaiwa wote ni wa Momposh.
Wanawake wakiwa na mapanga walimpeleka Momposh kwenye kituo cha polisi cha Kilgoris umbali wa kilomita sita na kuwakabidhi maafisa wa polisi.
Mwanaume huyo alipelekwa mahabusu na amepangiwa kwenda mahakamani jumanne ijayo.Sample za DNA zimechukuliwa kutoka kwa baba na mtoto na zimepelekwa maabara ili kujua ukweli wa mambo....
No comments:
Post a Comment