Huyu ni Msanii mkongwe maarufu kwa jina la Ray C ambaye leo hii ameamua kuyanadi mapaja yake akidai kwamba hiyo ndo sehemu muhimu ya mwili wake...Kila mwanamke ana mvuto wake, wapo wanaojivunia nyuso zao zenye macho yaliyoumbwa yakaumbika, nyuso zisizo na chunusi wala aina yoyote ya kovu...Wapo pia wanaojivunia makalio yao na sote tumekuwa tukishuhudia jitihada mbali mbali za akinadada za kujitengenezea makalio ya bandia ( ya kichina ) ili kujiongezea mvuto kwa wanaume.
Hali ni tofauti kidogo kwa msanii Ray C.Yeye anaamini kwamba mapaja ndo kila kitu na kwamba ni hicho kigezo muhimu kinachoangaliwa na wanaume wengi wa siku hizi...
"Nani asiyejua kwamba kuna makalio ya kichina? Umewahi sikia wapi mapaja ya kichina?..Haya tunayo wachache ambao tumejaliwa na muumba wetu".Hii ni kauli ya Ray C alipokuwa akipiga stori na mpekuzi wetu.
No comments:
Post a Comment