Wanawake wamekuwa wakihofia zaidi kwernda likizo ndefu za uzazi, wakiamini kwamba zimekuwa chanzo cha matatizo yao kazini na kutoa fursa kwa washindani wao kuchukua nafasi zao.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibunu na
kutolewa kwenye mtandao wa Dailyu Mail,robo tatu ya wanawake wenye mimba
wanaamini kwamba wamekuwa wakiziweka rehani kazi zao kutokana na likizo
hizo ndefu za uzazi.
Wanawake saba kati ya 10 waliohijiwa wameonyesha
kwamba wamekuwa wakiingiwa na mashaka ya kuwekwa kando kazini na
wamekuwa wakiziona kazi zao kuwa kitu cha thamani kuliko likizo
wanazochukua baada ya kujifungua.
Utafiti huo uliofanywa kupitia mtandao wa
maternitycover.com uliainisha kwamba kiwango cha juu cha woga kwa
wanawake wanaopata ujauzito huhusiana zaidi na namna ya kuendelea
kulinda ajira na taaluma zao.
Nusu ya wanawake 1,300 walioulizwa walieleza
kwamba wanaona ni vyema kuficha ujauzito kwa kutowaeleza wakuu wao wa
kazi hasa iwapo kuna nafasi ya kupata kazi mpya au kupandishwa daraja.
Sheria katika mataifa mengi zinaeleza kwamba
wanawake wanatakiwa kupewa wiki 26 (miezi sita) kama kiwango cha kawaida
kwa ajili ya likizo ya uzazi kwa kuwa nje ya kazi zao kisha kurejea.
Hata hivyo utafiti unaonyesha kwamba katika hali
ya saa ya uchumi wa ushindani, nusu ya wanawake wanaona kwamba wanaweka
rehani kazi zao kwa kuwa nje ya kazi kwa muda mrefu kwa ajili ya kuwa na
watoto wao.
Watatu katika kila wananwake wanne wanaofanya kazi
walisema ndoto za kupandishwa daraja hutoweka hasa wanapopata mimba na
kujifungua na mmoja katika kila watatu wanaamini kwamba kipindi hicho
hutoa fursa kwa wenzao kupandishwa madaraja badala yao.
No comments:
Post a Comment