Monday, 7 October 2013

Marekani: Al-Liby alikamatwa kihalali Libya

Marekani imesema kuwa gaidi aliyekamatwa na vikosi maalum vya Marekani nchini Libya anzuiliwa katika meli ya kijeshi katika bahari ya Mediterranea.
Abu Anas al Libi, anadaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda na amekuwa akisakwa kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Mareakni nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.
Waziriu wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alisema kuwa hakuna makosa kwa kumkamata Al Libi kwani alikuwa anasakwa kihalali kwa vitendo vya kigaidi
Awali viongozi wakuu wa Libya walitaka maelezo kutoka kwa Marekani, baada ya Abu Anas al Libi anayedaiwa kuwa mfuasi wa al-Qaeda kutekwa mjini Tripoli na makamando wa Marekani.
Mwanamme huyo, alikuwa anasakwa kwa kuhusika na mashambulio dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania miaka 15 iliyopita.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema Anas al Libi sasa anazuwiliwa nje ya Libya.

No comments:

Post a Comment