Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa amesema penalti aliyotoa
mwamuzi Mohamed Theofil na kuwapa sare 1-1 Simba iliwachanganya vijana
wake.Mkwasa alisema Simba haikustahili kupewa penalti licha ya kwamba
refa ndiye mwenye uamuzi wa mwisho na wao hawana budi kuukubali."Mechi
ilikuwa yetu na dhahiri tulikuwa tunaondoka na pointi tatu, vijana
walicheza vizuri, lakini baada ya Simba kupewa penalti wachezaji wangu
walionekana kuchanganyikiwa," alisema Mkwasa.
No comments:
Post a Comment