MWANADADA Ray C amesema kwa wakati huu anapenda mashabiki wake wamwite kwa jina jipya la Roho ya Paka kwani ndilo linamfaa.
Staa huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kama ‘Na
Wewe Milele’, ‘Sogea Sogea’, ‘Bila Sababu’ na nyingine nyingi amesema
jina hilo linamfaa kwani mambo aliyopitia kama isingekuwa roho yake
ngumu asingeweza kufika alipo sasa.
“Haikuwa kazi rahisi kuwa Ray C huyu wa sasa,
nimepitia wakati mgumu sana, walionipa moyo ni wachache kuliko waliokuwa
wakinikatisha tamaa, ndiyo maana nataka wajue kuwa mimi nina roho ngumu
kama ya paka,” alisema Ray C.
Akithibitisha kuwa ana roho ngumu, katika mtandao
wa instagram aliweka picha za zamani zinazomuonyesha akiwa amesinzia
baada ya kutumia dawa za kulevya na kuandika maneno ya kuwaasa watu
kujiepusha na dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment