KWENDA jela ni kitu cha mwisho ambacho binadamu yeyote
angetamani kimtokee katika maisha yake, lakini kitu hicho kimemtokea
supastaa wa Bongomovie, Davina anasema hawezi kulisahau tukio hilo.
Davina anayetamba na filamu ya Diana anasema
hawezi kulisahau tukio hilo ambalo ni moja kati ya yale mabaya
yaliyowahi kumtokea maishani.
“Kufikishwa jela si jambo dogo na halisahauliki
kamwe, lakini tunajifunza kutokana na vitu kama hivi ndiyo maana
ninataka kuitoboa siri hii kwa Watanzania kwa kuwatengenezea filamu,”
anasema Davina.
Filamu hiyo inachambua historia ya maisha ya Davina ibatabainisha mazuri na mabaya aliyopitia hili la kufikishwa Segerea.
“Unajua kuna watu wanavyotuona kwenye runinga huwa
hawafikirii kuwa na sisi tulipitia maisha yaliyojaa misukosuko, ukweli
ni kwamba mimi ni mmoja kati ya Watanzania waliopitia huko,” alisema
Davina.
No comments:
Post a Comment