MWANAMKE AMUIBA MTOTO WA MWENZAKE NA KWENDA KUMNYONYESHA,WAKATI ANAJUA ANA UKIMWI
Mwanamke mmoja
mzimbabwe ambaye
alimnyonyesha mtoto wa
jirani yake bila kibali/
ruhusa ya mama yake
anakabiliwa na miaka miwili gerezani kwa
kumwambukiza mtu
mwingine HIV kwa
kukusudia kwasababu
yeye ni mwathirika.
Mwanamke mwingine
mwenye umri wa miaka
39 Annie Mpariwa alifika
mahakama ya Gaborone
jumatano na kesi
ilipangwa october 24 ili wafanye vipimo vya HIV
kwa mara ya pili kwa
mtoto huyo.
Vipimo vya kwanza
vilionyesha kuwa mtoto
hajaathirika. Mpariwa alikamatwa wiki
iliyopita kwa kufanya
kosa dogo kwa
makusudi (ambalo ni
kumnyonyesha mtoto
bila kibali kutoka kwa mama yake) ila mtoto
akipimwa kwa mara ya
pili na kukutwa ni
mwathirika adhabu
itaongezwa na kuwa ya
'kumwambukiza mtu mwingine HIV makusudi'.
Mama wa mtoto huyo
mwenye miezi 14 alisema
kumuona jirani yake
akimnyonyesha ilikuwa
ni jambo la kushitusha sana kwake.
Aliendelea kusema kuwa
jirani yake alimchukua
mtoto wake aliyekuwa
nje na kwenda kumficha
chumbani kwake alikokuwa amepanga.
Baada ya kumtafuta
mtoto wake kwa muda
mrefu,alienda kugonga
hodi kwenye chumba cha
Mpariwa lakini hakujibiwa.
Alipochungulia dirishani
alimuona jirani yake
huyo ambaye ni
mwathirika wa ukimwi
akimnyonyesha mtoto wake.
"Nilipochungulia
dirishani nilimuona
akimnyonyesha
mtoto wangu.Nilipata
mshituko mkubwa
karibu nizimie",aliongezea kusema kwamba maziwa
ya jirani huyo yalikuwa
bado yanavuja na
inashangaza kwasababu
kwa muda huo yeye
hakuwa na mtoto ambaye anamnyonyesha
(hakuwa mzazi) wala
hakuwa mjamzito.
Tukio hilo limekuja
kwenye mwamko wa
sheria mpya zilizowekwa kuhusu HIV na AIDS
ambazo zimekuja na
adhabu kali kwa wale
wanaowaambukiza
wenzao virusi vya
ukimwi makusudi.
No comments:
Post a Comment