Wafuasi wa Kundi la Al-Shabaab nchini Somalia wamesema kuwa mji
wao Kusini mwa Somalia umeshambuliwa na wanajeshi wa mataifa ya
Magharibi.
Wapiganaji hao walisema wanajeshi wa kigeni waliuvamia Mji wa Barawe usiku wa manane.
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa helikopta ilitumiwa kwenye shambulio hilo.
Wengine wanaeleza kuwa wanajeshi waliingia usiku wakitokea maeneo ya pwani.
Al-Shabab ilisema shambulio hilo halikufanikiwa ingawa inakiri mpiganaji wao mmoja aliuawa.
Kundi hilo linadai kuwa wanajeshi maalumu wa
Uingereza na Uturuki ndio waliofanya shambulio lakini hayo yalikanushwa
na Uingereza na Uturuki.
Jina Al-Shabaab linamaanisha Kijana kwa
lugha ya Kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama Tawi la Vijana la Muungano
wa Mahakama za Kiislamu ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006.
Chanzo cha kuvunjika kwa muungano ni baada ya
kundi hilo lilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia
nchini Somalia kuunga mkono Serikali ambayo ilidaiwa kuwa ilikuwa ni
dhaifu.
No comments:
Post a Comment