Kijana mwenye umri wa miaka 24 akiwa ndani ya treni alitazama nje na kupiga kelele...
"Baba, tazama miti inarudi nyuma!" Baba alitabasamu.
Watu wawili waliokuwa wamekaa pembeni walimtazama kijana huyo mwenye
umri wa miaka 24 mwenye tabia za kitoto kwa huruma huku wakimsikitikia.
Ghafla kijana alipaza sauti tena... "Baba, tazama mawingu yanatufuata!"
Watu waliokaa pembeni walishindwa kujizuia, wakamwambia yule baba..."Kwanini usimpeleke kijana wako kwa daktari mzuri amtibu?"
Yule baba alitabasamu na kuwajibu..."Nimeshafanya hivyo na ndio kwanza
tumetoka hospitali, kijana wangu alizaliwa kipofu, leo ndiyo ameweza
kuona kwa mara ya kwanza..."
Kila mtu hapa duniani ana stori
yake. Usihukumu watu kabla hujawafahamu vizuri. Ukweli unaweza
kukushangaza...fikiria kabla ya kusema kitu...!
No comments:
Post a Comment