Serikali
imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu
kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze
kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.Kauli hiyo ilitolewa Dar es
Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philip Mulugo,wakati akizungumza na wanafunzi waliokosa mikopo ambapo
kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi wizarani hapo.
"Kasungura
kadogo na mkumbuke kuwa mkopo ni kuomba kuna kupata na kukosa...hivyo
wale waliokosa na walikuwa na vigezo watafute watu wengine wenye uwezo
wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata watume tena maombi," alisema.
Alisema
kilio chao amekisikia na leo atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
kuhusiana na malalamiko yao ambapo suala hilo litapelekwa Bungeni ili
kujadiliwa.
"Kama
Bunge litaamua kupunguza fedha kutoka kwenye bajeti zingine ili
kusomesha wanafunzi hao. Bunge litaamua kwani Serikali ina nia nzuri
sana kwani hadi sasa imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu
hawarudishi," alisema.
Alitaja
sababu nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia
uhitaji, kwani kuna masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu wa
wataalamu.
Alitaja
fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na wahandisi. Alitaja sababu
nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni waombaji kukosea majina na
vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa kwenye vyombo vya habari
warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.
Alisema
waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa 6,000 lakini waliorudi kufanya
marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000 walikuwa na vigezo lakini
wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).
Wanafunzi
waliokosa mikopo walisema kama wenzao wameweza kupata mikopo kwa
asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana ili wote waweze kupata
No comments:
Post a Comment