Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania (Bara), Philip Mangula ameshangazwa na chama
hicho kuwa na ‘jeshi’ kubwa la wanachama, lakini linazidiwa nguvu na
jeshi dogo la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hatua ambayo
imemfanya aamke na kusoma alama za nyakati kwa kuwarudia wananchi.
Akizungumza
na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na waandishi
wa habari jana kabla ya kuanza ziara yake jijini, Mangula alisema;
“CCM
ina jeshi kubwa la wanachama lakini linashindwa na jeshi dogo la
CHADEMA ambalo halina hata anuani... hivyo nimeona ipo haja kurudi kwenu
kuanzia ngazi ya chini kupitia matawi, shina na wananchi mnieleze
tatizo ni nini?”
Alisema
ili kufikia wananchi nkoani Dar es Salaam, atafanya ziara katika wilaya
zote za mkoa huo na kukutana na watendaji, wanachama na wananchi kwani
kila mwana CCM ni askari wa mstari wa mbele, lakini anashangazwa na
nguvu ndogo iliyopo sasa.
“Chama
kikiwa na nguvu ndipo na Serikali inavyokuwa na nguvu, umefika wakati
tuelewe kuwa ni muhimu chama kiwasemee watu na si viongozi wa chama
wakisemee; hivyo uhai wa chama ni jambo muhimu kwa wana CCM,” alisema
Alieleza
kuwa makundi yaliyotokana na uchaguzi wa 2010 ndani ya chama hicho,
bado yapo na yanaendelea kwa kasi, hali iliyoathiri zaidi Chama mpaka
kufikia mwaka 2012, hivyo mkakati wa kujua vipi yaondolewe pasipo
kuathiri zaidi 2014 mpaka 2015 unahitaji kuwepo na mipango imara.
Mangula
alisema katika ziara yake hiyo ya mafunzo ambayo imetokana na kutambua
kuwa nguvu ya chama ni uwepo wa wanachama, atatenga muda mwingi
kuzungumzia changamoto zinazowakabili na kuwagawa wana CCM.
Alisema
kwa kufanya hivyo atapata sababu zinazokwamisha maendeleo ya chama
hicho. Alihimiza wana CCM kuelewa kuwa katika wiki ya maadhimisho ya
kumbukumbu ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, ipo haja
kuenzi harakati zake kwa kukiongezea nguvu chama.
Mangula alisema kujenga chama kunahitaji kujitoa hata kufikia kuacha nafasi ya madaraka kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.
“Wakati
wa wiki ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni muhimu kuwa na chama chenye
nguvu na kujitoa kwani Mwalimu aliacha hata nafasi ya Uwaziri Mkuu na k
umuachia Mzee Rashid Kawawa kwa lengo la kurudi katika kazi za ujenzi
wa chama na pia tukumbuke Mwalimu aliacha kazi ya Urais mwaka 1985 na
nafasi yake kuchukuliwa na Rais Mwinyi, ambapo yeye alirudi tena kufanya
kazi za chama hivyo kukijenga chama kunahitaji kujitoa ili kiweze kuwa
na nguvu kubwa,” alisema
No comments:
Post a Comment