Wednesday 21 August 2013

Arsenal yaichapa Fenerbahce 3-0


Walipua mizinga wa Kaskazini mwa London, Arsenal wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya hatua ya makundi.

Arsenal iliyokuwa ugenini huko nchini Uturuki imeichapa Fenerbahce nyumbani kwao 3-0 katika mchezo ambao ulishuudia kipindi cha kwanza kikimalizika bila Pasi nzuri kutoka kwa Aron Ramsey iliyomkuta Theo Walcott ambaye bila kusita naye aliunganisha hadi kwa Kieran Gibbs aliyelitazama lango la Fenerbahce na kuandika bao la kwanza kwa Arsenal kunako dakika ya 51 ya mchezo.
Dakika chache baadaye Arsenal waliendelea kulisakama lango la Fenerbahce, lakini Aron Ramsey aliongeza matumaini ya kutopoteza mchezo wa pili na kuwapa raha mashabiki wa Ashburton Grove kwa kufunga bao la pili.
Pengine bao la pili liliwachanganya zaidi Fenerbahce ambao licha ya kucheza mechi hiyo bado wapo kwenye adhabu ya kutoshiriki michuano yoyote ya ulaya lakini rufaa waliyoikata ambayo itasikilizwa tarehe 28 mwezi wa Agosti inawafanya waruhusiwe kuendelea na mashindano.
Kinda mwiingereza Theo Walcott alikuwa mwiba kwa Fenerbahce, kwani kunako dakika ya 75 alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la kumi na nane na mwamuzi wa kati aliamuru ipigwe penati ambayo mfaransa Olivier Giroud aliipiga na kuandika bao la tatu na la mwisho kwa Arsenal.
Matoke ya mechi nyingine za kufuzu klabu bingwa ulaya, Dinamo Zagreb ilikubali kichapo cha bao 0 - 2 nyumbani kutoka kwa Austria Wien.
Ludogorets nayo ikatandikwa 2 - 4 na FC Basel ya Uswis, wakati Steaua Bucureşti ilitoshana nguvu na ya 1 - 1 na Legia Warszawa na Schalke 04 ya ujerumani nayo ikashindwa kutamba nyumbani baada ya kutoka sare tasa ya 1 - 1 PAOK.
Arsenal wameshiriki michuano ya klabu bingwa ulaya kwa miaka 14 mfululizo bila kukosa.
Michezo ya marudaniano itapigwa tarehe 27 Agosti. za timu zote kuguswa.

No comments:

Post a Comment