Thursday, 22 August 2013

MZEE GURUMO ASTAAFU MUZIKI


Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo leo amestaafu rasmi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.

Mzee Gurumo amesema “Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu”.

Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo amesema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.

Amesema ameimba kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli hana, hata hivyo Mzee Gurumo akasema anashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.

No comments:

Post a Comment