Hatimaye beki wa kimataifa wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Shomary Kapombe amefuzu majaribio aliyokuwa akifanya barani ulaya kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya AS Cannes ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mwandishi wa BBC - Abdul Mohamed ni kwamba Shomary Kapombe amefuzu majaribio hayo na sasa zimebakia taratibu tu za uhamisho ili ajiunge rasmi na timu hiyo ya AS Cannes inayoshiriki kwenye ligi daraja la nne nchini Ufaransa.
Kapombe aliondoka nchini takribani mwezi mmoja uliopita na kwenda barani ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Mtandao huu upo katika kujaribu kufanya mawasiliano na uongozi wa Simba ili kupata taarifa rasmi juu ya usajili huu wa Shomary Kapombe.
No comments:
Post a Comment