Wednesday 21 August 2013

Rais Kikwete afanya Mabadiliko ya Makatibu Wakuu wa Wizara

Nimepata taarifa toka Ikulu kuwa Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue anatangaza makatibu wakuu wa wizara na manaibu wao wapya leo hii.

Haya yatakuwa mabadiliko makubwa tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 na wengi wa sasa watatemwa. 

Nitawaletea orodha yote very soon hapa.

Updates:

Mkutano baina ya CS Ombeni Sefue na waandishi wa habari kutangaza Makatibu wakuu wapya na Naibu Makatibu wakuu kitafanyika Ikulu saa 10 kamili Jioni leo.

UPDATES:

Baadhi ya walioteuliwa:

Dr Florence Turuka - Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi Joyce Mapunjo -Katibu Mkuu wizara ya Afrika Mashariki
Bw Sihaba Mkinga -Katibu Mkuu -Habari, Michezo na Utamaduni
Bi Sofia Kaduma -Katibu Mkuu Kilimo na Ushirika
Dr Deo Mtasiwa -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu akishughulikia Afya

Majina Mengine nitawaleteeni baadae.

Patrick Rutabanzibwa Amestaafu kwa hiari.

Wafuatao wameondolewa Ukatibu Mkuu na badala yake watapangiwa kazi nyingine (Ubalozi???)

1. Seth Kamuhanda
2. Kijakazi Mtengwa
3. Omary Chambo

Bw Peniel Lyimo aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu amehamishiwa Ofisi ya Rais kuwa Naibu Mtendaji Mkuu Kitengo cha PDU akishughulikia maswala ya Kilimo

MORE UPDATES 
Orodha kamili ya walioteuliwa ni:

Jumanne Sagini amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.
Dk. Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,awali alikuwa Naibu Katibu 

Dk. Patrick Makungu- Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo
Alphayo Kitanda- Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Dk. Shaaban Mwinjaka - Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, 
Dk.Uledi Mussa-Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Profesa Sifuni Mchome- Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.

Charles Pallangyo - Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu
Anna Maembe -Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo
Sihaba Nkinga- Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo
Sophia Kaduma- Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.



Naibu makatibu wakuu wapya walioteuliwa ni:

Angelina Madete- Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,
Regina Kikuli -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Zuberi Sumataba -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia suala la elimu
Edwin Kiliba -Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI.

Dk. Yamungu Kayandabila -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,
Profesa Adolf Mkenda -Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia sera,
Dorothy Mwanyika -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni.

Rose Shelukindo -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Dk. Selassie Mayunga -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Monica Mwamunyange -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,
Consolata Mgimba -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Profesa Elisante ole Gabriel Laizer -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Armantius Msole -Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Waliopewa uhamisho kuwa ni:

John Mngondo amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi,
Selestine Gesimba - Wizara ya Maliasili na Utalii anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais.

Maria Bilia -Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi 0
Nuru Milao anahamia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na W-atoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

Hiyo ndio orodha yote ya walioteiuliwa, kuhamishwa na kuacha kazi pia.


Chanzo JF

No comments:

Post a Comment