Monday 19 August 2013

Vigogo kutoa ushahidi dhidi ya Mbunge Lema


Mkuu wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha, John Nanyaro na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Gillis Mroto, leo wanaanza kutoa ushahidi katika kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Mashahidi wengine katika kesi hiyo ni, Mkaguzi wa Polisi Bernard Nyambanyana na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane.
Hali kadhalika PC Godfrey na Joachim Mahanyu . Wakili wa Serikali, Elinenya Njiro, alitaja mashahidi wengine watakaotoa ushahidi wao mahakamani kuwa Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu Hamidu, wote kutoka Chuo cha Uhasibu.
Lema anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, alikwenda katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha, mithili ya mtu aliyekwenda kwenye send-off na kwamba hajui chuo hicho kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho.
Wakili Njiro alidai kuwa mbunge huyo alitenda kosa hilo Aprili 24 mwaka huu, akiwa katika eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu na kwamba kitendo hicho kinapingana na kifungu cha 390 sura ya 35 ya sheria ya kanuni ya adhabu.

No comments:

Post a Comment