Saturday, 17 August 2013

Jaji wa mahakama kuu Uingereza ameagiza mwanamme mmoja aliye na matatizo ya kuelewa mambo kwa haraka kuhasiwa.

Hospitali ya Uingereza
Mwanamme huyo ni mzazi wa mtoto mmoja na anaishi eneo la Midlands. Jaji Eleanor King amesema ilikua sawa kwa mwanamme huyo kuhasiwa baada ya kusikia kwamba mwanamme huyo angepata mafadhaiko endapo angempata mtoto wa pili.
Wataalamu wa kiafya wamesema mwanamme huyo alielewa masuala ya mapenzi, lakini hakuelewa masuala ya mpango wa uzazi.Madaktari walisema mwanamme huyo kwa jina DE hangeaminiwa kutumia mipira ya Condom au njiya nyingine za mpango wa uzazi.
Mahakama ya London inayoshughulikia masuala ya uzazi imesikiza tetesi za mwanamme huyo ambapo amesema hataki kupata mtoto mwingine. Mahakama iliingilia kati ili kuamua baada ya mwanamme huyo kushindwa kuamua njia gani ya mpango wa uzazi zlistahili kupata.
Kesi hii ya kuhasiwa iliwasilishwa na bima ya mwanamme huyo pomoja , wazazi wake na huduma ya jamii inayomtunza. Hii ndio mara ya kwanza mahakama ya Uingereza imeagiza mwanamme kuhasiwa kwa maslahi yake na jamii.

No comments:

Post a Comment