Thursday, 22 August 2013

HITILAFU KATIKA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME YA SONGAS JIJINI DAR


HABARI zilizotufikia leo alfajiri ni kwamba palitokea hitilafu katika mitambo ya gesi inayozalisha umeme ya Songas iliyopo Ubungo hali iliyopelekea umeme kukatika jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda aliyekuwepo jirani na eneo la tukio majira ya saa 11 alfajiri, alidai kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliokuwa unatoka eneo hilo hali iliyopelekea wananchi waliokuwa jirani kukimbia huku wakijifunika usoni maana moshi huo ulikuwa unawasha. "Ilikuwa ni vigumu kumuona mtu wa mbele yako kwa wakati huo maana moshi ulikuwa mkubwa" alisema shuhuda huyo. Kwa sasa hali ni shwari eneo hilo baada ya jitihada za zimamoto japo maeneo mengi ya mji bado umeme haujarudi.

No comments:

Post a Comment