Tuesday, 20 August 2013

KALIPIO LA MWIGULU KWENDA KWA MWANA CHADEMA;ONYO KALI KWA JESCA KISHOA(CHADEMA) KUNITUKANA JIMBONI KWANGU IWE MWANZO NA MWISHO.


Ndugu,
Jesca Kishoa,Nimepata habari na mkanda mzima wa mikutano yako ya kufungua matawi ya CHADEMA wilaya ya Iramba.
Umetumia siku nzima kunitukana,kunizushia na kuwazuia wananchi wangu kushiriki shughuli za maendeleo ya wilaya yao.
Sijajua kama ulitumwa kuja kunitukana ama ni Utashi wako.
Ninachotaka kukushauri usimfuate tena mamba kwenye kina kirefu cha maji.Hata wakubwa wako wote,chama kizima huu mziki ulishawashinda na bado wanahangaika nao kila siku bila mafanikio na katu hawata fanikiwa.!

Nimeona nikushauri tu kuwa unaweza kufungua matawi ya chama chako kila kitongoji au kila mtaa lakini usirudie matusi kwangu na wala usirudie kuwashawishi wananchi wangu washishiriki shughuli za maendeleo kwa jina la kuwafundisha Elimu ya uraia.
Wilaya ya Iramba tumejenga maabara shule zote za kata(Boma za maabara) wewe hutaki kushiriki.
Tumefungua miradi ya maji kadhaa na mingine ipo kwenye hatua za mwisho katika vijiji na kata mbalimbali!
Tumejenga barabara za kuunganisha Wilaya ya Iramba yote iweze kupitika wakati wa masika na kiangazi!

Tumejenga zahanati,tunaongoza kwa mwaka wa pili mfululizo kwa huduma safi za Afya!
Tunafanya jitihada kuinua michezo ndani ya wilaya yetu,

Tumezungusha umeme wilaya ya Iramba na sasa tunapeleka umeme vijiji vyote vya Iramba.
Hivi CHADEMA mkoje,bila shaka hamna wazo mbala kwa maendeleo ya Wanairamba na Taifa hili mnaishia kutukana?

Wambie na waliokutuma msifungue matawi tu,jengeni makao makuu ya CHADEMA Kiomboi halafu tukutane kwenye uchaguzi.
Ukipata hata nusu ya kura zangu nitaandika barua kwenda tume wakutangaze Mbunge.
Look at You YoungLady>>>>UNAPOTEZA MUDA WAKO,UNAPOTEZA NGUVU NA UWEZO WAKO WA KUFIKIRI KWA KAZI HII YA KUNITUKANA,HUNA LA KUFANYA?UNAWINDA TEMBO KWA MANATI?

Nimekuonya kwaajili ya Matusi yako hayo.
TUTAHESHIMIANA

No comments:

Post a Comment