Tuesday 20 August 2013

Dk. Shein apangua Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kufuatia marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.

Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya MzeeMarekebisho ya muundo na shughuli katika baadhi ya Wizara ni kama ifuatavyo.


  1. Shughuli za Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ zimeondolewa katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuundiwa Wizara mpya.
  2. Shughuli za Utawala Bora zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
  3. Shughuli za kazi zimeunganishwa na shughuli za utumishi na kuundiwa Wizara mpya.
  4. Shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika zimeondolewa kutoka Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika na kuunganishwa na shughuli za ustawi wa jamii, vijana, wanawake na watoto.
  5. Shughuli za Tume ya Mipango zimeondolewa kutoka Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
  6. Idara ya Uratibu na Shughuli za SMZ, Dar es salaam imeondolewa kutoka Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na kuhamishiwa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais.


Kufuatia marekebisho hayo, zimeundwa Wizara mpya nne ambazo ni (i) Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ (ii) Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma (iii) Wizara ya Fedha na (iv) Wizara ya uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto.

Kufuatia kuundwa kwa Wizara hizo mpya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya kifungu 44 (1) na kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Wizara kwa kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo.

1.
Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

a) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame.
b) Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Nd. Salum Maulid Salum
c) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Nd. Said Abdalla Natepe.
2. Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ

a) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheir
b) Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Nd. Joseph Abdalla Meza
c) Naibu Katibu (Tawala za Mikoa) Nd. Mwinyiussi A. Hassan
d) Naibu Katibu Mkuu (Idara maalum za SMZ) CDR Julius Nalimy Maziku

3 Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma 

a) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa umma Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman
b) Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Nd. Fatma Gharib Bilal
c) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Nd. Yakout Hassan Yakout

4 Wizara ya Fedha

a) Waziri wa Fedha Mheshimwa Omar Yussuf Mzee
b) Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Khamis Mussa Omar
c) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd. Juma Ameir Hafidh.

5 Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto

a) Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Mheshimiwa Zainab Omar Mohamed.
b) Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Nd. Asha Ali Abdalla.
c) Naibu Katibu Mkuu (Uwezeshaji na Ushirika) Nd. Ali Khamis Juma
d) Naibu Katibu Mkuu (Ustawi wa Jamii, Vijana,Wanawake na Watoto) Nd. Msham Abdalla Khamis.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment