Takriban watu 37 wakufa baada ya kugongwa na treni wakati wakivuka njia ya reli katika jimbo la Bihar, India. Maafisa wamesema wengi wa abiria walikua mahujaji wa Ki-Hindi waliokua wametua katika kituo kimoja cha eneo la Dhamara Ghat na walikua njiani kuelekea Hekalu iliyoko Wilaya ya Saharsa.
Ajali hiyo ilipelekea ghathabu ya raia ambao waliteketeza mabehewa ya treni hiyo. Makundi ya wokozi yanaendelea kutafuta manusura na polisi wa kuzima ghasia wametumwa eneo la ajali.
Mkuu wa pilisi katika jimbo la Bihar amesema haijathibitishwa idadi kamili ya watu waliokufa, kwani vipande vipande vya miili ya watu imetapakaa eneo hilo.
Maafisa wa huduma ya reli wamesema treni hiyo ya mwendo wa kasi ilikikuwa njiani na haikutarajiwa kutua kituo cha Dhamara Ghat. Hata hivyo ilisimama baada ya ajali kutokea ambapo umati wa watu ulishambulia dereva na kumjeruhi vibaya.
Huduma ya treni inamilikiwa na serikali nchini India na inawahudumia abiria milioni 18 kila siku.Serikali imesema zaidi ya watu laki moja unusu waliuawa na treni mwaka jana pekee wakati wakivuka njia ya reli inayotumika na treni za mwendo wa kasi.
No comments:
Post a Comment