MBUNGE wa Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Lameck Nchemba amenaswa tena, safari hii akimlisha chakula mtoto wake mchanga akiwa kitandani ‘on bed’.
Katika picha hiyo iliyonaswa hivi karibuni mtandaoni imemuonesha mbunge huyo akiwa hotelini ikiwa imetupiwa maneno: “Malezi kusaidiana.”
Ilidaiwa kuwa ‘sosi’ ya kusambaa kwa picha hiyo ni yeye mwenyewe ambaye aliitupia kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo ilipata maoni mengi ya wadau waliokuwa wakimsifia na wengine kuitilia shaka kuwa ni usanii.
Kuonesha kuwa anayajua malezi, Mwigulu alikuwa ametenga pampasi pembeni kwa ajili ya kumbadilishia mwanaye kwani watoto wachanga hujisaidia mara kwa mara huku akiendelea kumlisha uji kwa kijiko.
Wadau hao wa mheshimiwa huyo mtandaoni wapatao 306 waliipenda ‘like’ picha hiyo wakimpongeza kwa uamuzi wake wa kusaidiana na mwenzi wake katika kulea mtoto.
Mwezi uliopita, mbunge huyo alianikwa mtandaoni akiwa na familia yake, mke na watoto watu huku akiwa amembeba mmoja mgongoni na kuibua gumzo kubwa.
No comments:
Post a Comment