Wednesday, 21 August 2013

Silaha za sumu zawaua mamia Syria

Maiti za raia waliouawa SyriaMamia ya raia wameuawa kufuatia shambulio lililotumia silaha za kemikali viungani mwa Mji Mkuu wa Syria, Damascus. Makundi ya upinzani yanasema makombora yaliyokua na kemikali ya sumu yalilenga eneo la Ghouta usiku wa kuamia Jumatano.
Inadaiwa majeshi ya serikali yalikua yakiwashambulia waasi.Hata hivyo Shirika la utangazaji la serikali limetaja taarifa hizo kama upuzi mtupu,na kusema ni kisingizio tu cha kuwachochea wakaguzi wa Umoja wa Mataifa walioko Syria.
Muungano wa upinzani umesema zaidi ya watu 650 waliuawa katika shambulizi hilo.Makundi mengine ya kiraia pia yametangaza vifo vya mamia katika shambulio hilo japo taarifa hizo hazijathibitishwa kirasmi.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, ametaka utawala wa Syria kukubalia wakaguzi wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo na kusema Uingereza itawasilisha hoja katika Umoja wa Mataifa.
Muungano wa nchi za Kiarabu pia umeunga mkono wakaguzi hao kuingia eneo hilo.Shambulizi hilo ni moja wapo ya operesheni kali ya jeshi la serikali katika maeneo yanayothibitiwa na waasi mjini Damascus.
Maeneo yaliyoathirika na shambulio la karibuni ni pamoja na Irbin,Duma na Muadhamiya.

No comments:

Post a Comment