SERIKALI imepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha usimamizi wa mazingira.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Terezya Huvisa, alipozungumza na waandishi wa bahari na kuongeza kuwa, watu wote ambao watabainika kuzalisha au kuuza mifuko hiyo, watachukuliwa hatua.
Alisema Serikali imechukua hatua hiyo ili kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia katika uchafu wa mazingira.
"Zuio hili linahusu mifuko yote ya plastiki ya kubebea bidhaa kutoka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni 100 inayooza na vifungashio vya bidhaa mbalimbali kama vifaa vya hospitalini," alisema.
Aliongeza kuwa, agizo hilo linapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, maduka na wananchi ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira.
Dkt. Huvisa alisema, awali Serikali iliruhusu matumizi ya mifuko yenye unene usiopungua maikroni 30, lakini kutokana na wananchi kutokuwa na uwezo wa kupambanua unene huo, wafanyabiashara walitumia mwanya huo kuchanganya mifuko hiyo.
Alisema tatizo la kuingia kinyemela kwa mifuko ya plastiki nchini linaongezeka kwa kasi hivyo ni tatizo linaloikumba nchi zote za Afrika Mashariki.
" J i t i h a d a z i n a h i t a j i k a k u h a k i k i s h a a g i z o h i l i linazingatiwa, misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii itafanyika maeneo yote ndani ya nchi na watakaokamatwa watachukuliwa hatua," alisema.
Alisema mswada wa kupiga marufuku mifuko yote ya plastiki, uliwasilishwa katika Bunge la Afrika Mashariki na kupitishwa na Bunge hilo Februari 3,2012.
Mswada huo uliridhiwa na marais wote wa nchi wanachama kwa lengo la kupiga marufuku matumizi ya baadhi ya bidhaa za plastiki zinazochangia kuchafua mazingira.
No comments:
Post a Comment