Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amewaomba polisi kuyakabili magenge yanayoiba nywele za wanawake. Baadhi ya waathiriwa wamesema walinyolewa nywele zao kwa lazima ambapo magenge yaliwatisha kuwapiga risasi.
Visa vya wizi wa nywele vimeongezeka katika mji wa pili mkubwa nchini Venzuela wa Maracaibo. Nywele hizo huuzwa kwa maduka ya usuzi kutumika kama nywele bandia kwa wanawake.Rais Maduro aliwaita wezi hao kama "magenge yanayokata nywele za wanasichana".
Wanawake wamesema wamekua wakitishwa kushika nywele zao tuta moja ili kuwezesha wezi hao kuzinyoa kwa urahisi.Hata hivyo mwandishi wa BBC nchini Venezuela amesema polisi hawajapokea malalamishi yeyote.
Mmoja wa waathiriwa amesema aliogopa kutoa ripoti kwa polisi kwa kuogopa kuchekwa kwa kuwa kupara.
No comments:
Post a Comment