Viongozi wa Kanda ya Kusini mwa Afrika wamezitaka dola za Magharibi kuondoa vikwazo vilivyowekewa nchi ya Zimbabwe, baada ya kuithinisha ushindi wa Rais Robert Mugabe.
Rais wa Malawi Joyce Banda ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Muungano wa SADC amesema raia wa Zimbabwe ndio wanaoumia na vikwazo hivyo.Rais wa Malawi Joyce Banda ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Muungano wa SADC amesema raia wa Zimbabwe ndio wanaoumia na vikwazo hivyo.Muungano wa Ulaya na Marekani ziliwekea Zimbabwe vikwazo mwaka wa 2002 baada ya kulalamikia utawala wa Mugabe kwa kuwakandamiza wapinzani wake. Hata hivyo Mugabe amekanusha madai hayo. Rais huyo wa Zimbabwe anatarajiwa kuapishwa upya Alhamisi ya wiki hii.
Tayari Mugabe na washirika wake tisa ambao ni maafisa wa chama tawala cha Zanu-PF wamewekewa vikwazo vya usafiri na Muungano wa Ulaya. Pia kampuni kadhaa zimepigwa marufuku kufanya biashara na Muungano huo.
Marekani pia imeweka vikwazo kwa Mugabe dhidi ya kuzuru nchini humo na kuharamisha kampuni shirika za Mugabe dhidi ya kufanya biashara na Washington.
Robert Mugabe alishinda Urais kwa asili mia 61 dhidi ya Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai aliyezoa asili mia 34 ya kura za Urais. Ijumaa wiki jana chama cha Tsvangirai cha MDC kiliondoa kesi mahakamani ya kupinga uchaguzi huo kikidai mahakama haiwezi kutekeleza haki.
MDC kilidai uchaguzi mkuu huo ulikumbwa na udanganyifu, madai yaliyopingwa na Muungano wa Ulaya na waangalizi wa kimataifa. Katika mkutano wa nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika, SADC ilisema kwamba Zimbabwe imefanya uchaguzi huru na haki na wakati umefika kwa vikwazo vya sasa kuondolewa.
Muungano wa Ulaya umesema uchaguzi wa Zimbabwe ulikua wa amani lakini kulikua na visa vya udanganyifu. Mugabe ametawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1980.
No comments:
Post a Comment