MBINU ALIJOTUMIA WAZIRI MKUU WA NORWAY KUPATA MAONI KUTOKA KWA WANANCHI

Waziri Mkuu wa Norway Bw. Jens Stoltenberg alitumia masaa kadhaa jijini Oslo akiendesha Taxi kwa siri huku akiwa amevalia miwani myeusi na mavazi maalumu ya madereva wa Taxi, lengo kuu likiwa ni kusikia maoni ya raia kuhusiana na mambo kadhaa yanayoendelea nchini humo.
Waziri Mkuu huyo alisema anaamini mazungumzo mengi ambayo hufanya na madereva wa taxi na abiria wao huwa na ukweli zaidi wa kile ambacho raia wanakitaka.
Hata hivyo, baada ya kubeba raia kadhaa, 'dili' likabumbuluka na raia kugundua kuwa dereva aliyekuwa anawabeba ni Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment