Warembo wanaotarajia kushiriki Redd’s Miss Ilala Talent hii leo, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
**********
KATIKA Kuelekea Redds Miss Ilala Ijumaa, leo kutakuwa na shindano la kumtafuta mrembo mwenye kipaji (Talent) itakayofanyika katika mgahawa wa City Sports and Loungeuliopo katikati ya jiji.
Mratibu wa shindano hilo, Juma Mabakila alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa warembo wote 14 wamejipanga kuonesha vipaji vyao ipasavyo.
Mabakila alisema mshindi wa talent atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa ijayo katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower ulipo katikati ya jiji.
No comments:
Post a Comment