
Uongozi wa klabu ya Yanga umeahirisha mkutano wa dharura wa wanachama wote uliokuwa ufanyike siku ya jumapili tarehe 18.08.2013 katika viwanja vya sabasaba ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam saa 3:30 asubuhi kujadailiana juu ya suala la Azam TV kurusha michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu kwa niaba ya makamu mwenyekiti wa Yanga, katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amesema mkutano huo umeahirishwa kufuatia kuwepo kwa kikao kati ya Naibu Waziri wa habari, utamaduni, vijana na michezo mhe. Amos Makalla na viongozi wa kamati ya Ligi, TFF, Azam Media na viongozi wa klabu ya Yanga
No comments:
Post a Comment