Sunday, 11 August 2013

Wasafirishao wakimbizi kimagendo wabanwa

Polisi wa Uspania wanasema kwamba wamelikamata gengi linalosafirisha wahamiaji kimagendo.
Ushahidi uliopatikana na polisi wa Uspania dhidi ya wahalifu wanaosafirisha wahamiaji kimagendo

Msemaji alieleza kuwa gengi hilo likiwasafirisha raia wa Uchina na kuwaingiza kimagendo katika nchi za Ulaya na Marekani, na kila mkimbizi akilipa kama Euro 50,000 kwa safari hiyo.Watu 75 wametiwa mbaroni Uspania na Ufaransa.
Polisi wanasema viongozi wa gengi hilo Ulaya waliokuwa na makao yao mjini Barcelona, ni kati ya wale waliokamatwa.
Polisi piya wamekuta paspoti zaidi ya 80 za nchi kama Japan, Hong Kong na Singapore.

No comments:

Post a Comment