Kiungo huyo awali kabla ya kwenda Azam FC msimu wa 2009/2010 akiwa anaichezea timu hiyo, alikuwa anavaa jezi hiyo na baadaye aliivaa pia alipokuwa Simba, lakini baada ya kurejea Yanga amekwaa kisiki kwa kuwa inatumiwa na Nizar.
Ngassa ambaye amerejea Yanga hivi karibuni, alikabidhiwa jezi namba 9 akaikataa, akabadilishiwa na kupewa namba 17 lakini nayo ameikubali kwa shingo upande kwa kuwa haitaki pia.
Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Ngassa anataka kurejeshewa jezi hiyo lakini uongozi unashindwa jinsi ya kuichukua kutoka kwa Nizar ambaye ni kiungo mkongwe.
Gazeti hili lilipomuuliza Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh kuhusu sakata hilo alisema awali jezi namba 16 ilikuwa ikivaliwa na Rashid Gumbo lakini alipoondoka akapewa Nizar.
“Ngassa aliporejea (Yanga) akataka apatiwe jezi yake namba 16, lakini imeshindikana kumpa jezi hiyo kutokana na kuwepo mchezaji mwingine anayeivaa, tukampa namba tisa aliyoivaa mara moja kisha akaikataa tukamshauri avae namba 17.
“Licha ya kumpa namba 17, anaonekana kutoridhishwa nayo, badala yake anaitaka namba 16. Uongozi ni ngumu kumvua Nizar labda wakubaliane wenyewe,” alisema Saleh.
No comments:
Post a Comment