Saturday, 17 August 2013

RAY C AWAFUNGULIA NJIA MATEJA KWENDA IKULU

Kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kumuita ikulu mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ kisha kumsaidia kumtoa kwenye dimbwi la utumiaji wa madawa ya kulevya, kimesababisha kiongozi huyo wa nchi kulazimika kuwaita na mateja wengine ili kuzungumza nao.Mateja hao wanaopatiwa matibabu kwenye Kituo cha Pili Missana Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar, walitinga Ikulu Jumanne iliyopita huku wakiwa wameongozana na mfadhili wa kituo hicho, Zachakia Hans Poppe pamoja na wadau wengine.
Akizungumza na Ijumaa juzi, mmoja wa wakurugenzi wa kituo hicho, Pili Missana alisema wamefarijika sana kupata mualiko huo na wanaamini ni hatua mojawapo kuelekea kwenye kulikabili vilivyo tatizo la matumizi ya ‘unga’ nchini.Naye Rais JK katika kukisaidia kituo hicho, ameitaka Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Magonjwa ya Akili na Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya kushirikiana nacho ili kiweze kuwasaidia vijana wengi kadiri inavyowezekana.

No comments:

Post a Comment